KIBANDA CHA KUFUGIA
Tunasaidia
kwenye ujenzi wa vibanda bora vya sungura, kwagharama ya Tshs 65,000/= tu kwa kimoja cha ukubwa
wa futi 2.53 , chenye
uwezo wa kufugia
Sungura mmoja mkubwa
wakuzalisha pamoja na watoto wake kwa mwezi mmoja baada
yakuzaliwa yaani kipindi chote cha unyonyeshwaji, na kibanda cha saizi hiyo pia
kinaweza kufugia hadi sungura kumi wa umri wa miezi mitatu.
Tunashauri
ujenzi wa vibanda vitatu kwa kila jike (kupata nafasi ya watoto wanaomaliza
kunyonya kwani jike huzaa kila baada ya miezi 2) na pia kibanda kimoja kwa kila
dume.
MBEGU
Tunawataka wakulima wetu kufuga mbegu
bora na halisi ya sungura watakaotupa nyama bora kwa soko letu, na
tunawauzia kwa gharama
ya Tshs 80,000/= kwa
kila jike aliyetayari
kubeba mimba na
Tshs 40,000/= kwa kila dume
mwenye umri wakuzalisha.
MAFUNZO YETU
MAFUNZO YETU
Tuna
mafunzo mara kwa
mara pia, na zaidi kuhusu
ujezi wa mabanda
bora, Utunzaji na
ufugaji kwa ujumla, na kuhusiana
na maswala ya magonjwa na namna yakuzuia.
Tuna
saini mkataba na mkulima/mfugaji (kwa
ada maalum kila
mwaka) ambao utamuhakikishia mfugaji/mkulima soko kwa kipindi chote cha mkataba pale sungura wake wanapokuwa tayari kwa
kuuzwa.
Tunanunua sungura katika umri wa miezi
4-5. Kwa umri huo sungura mwenye afya aliyelishwa vizuri anapaswa kuwa na uzito
wa kilo 3-4, na kilo moja ya sungura akiwa hai tunamnunua kwa Tshs 8,000/=.
Tafadhali
wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.
Tafadhali
zingatia mafunzo kwa mtunzaji wa sungura wako/au kama ni wewe mwenyewe ni ya
muhimu kujifunza mambo ya msingi unapoanza mradi nasi,
Paleunapohitaji
ushauri wa kitaalam utagharimia nauli ya mtaalamu atakufundisha UFUGAJI BORA WAKISASA kwa vitendo.
17 comments
Write commentsjambo
ReplySijambo doctor ninahitaji kufuga Ila nipo Dodoma inawezekana
Replyhabar dr. naitwa rashidi nipo dodoma nahitaji kufuga sungura kibishar nmaweza pata muongozo wako please
ReplyNaweza pata msfunma zaidi
ReplyNiko Morogoro Ifakara. Je ninaweza kupata nafasi kwa mafunzo ya mwangalizi wa sungura halafu ninunue majike? 0784453115
ReplyNiko Morogoro Ifakara. Je ninaweza kupata nafasi kwa mafunzo ya mwangalizi wa sungura halafu ninunue majike? 0784453115
ReplyDoctor nngependaa kupata mawasiliano na ww binafsi namba zangu n 0678278404 na pia email yangu n Bboymax129@gmail.com ningependaa tuwasiliane naitwa max namengi yakuzungumzaa mtaalamu
Replyhabari daktari nipo mlandizi na ningependa kuanza rasmi ufugaji wa sungura kibiashara naomba mwongozo.Anuani pepe ni ahimidiwe@gmail.com
Replynyie mnaniuzia sungura kwa 80,000 halafu mie sungura huyo nakuuzia wewe kwa kilo 8000 akiwa na kilo 4 unamnunua 32000, mimi namkuza mpaka anafikia umri wa miezi 4 inamaana huyo sungura atakuwa na muda mfupi wa kushika mimba, mimi mkulima nafaidikaje?
ReplyHabari mtaalamu. Naomba namba zako za simu. Napatikana kwa pkilasara@yahoo.co.uk
ReplyNaomba michoro ya banda LA sungura, nitanunua sungura Wa kuanzia.
ReplyJaribuni kutokumnyonya sana mkulima.... Angalau kila moja iwe 12000/= maana nyie baada ya mwezi mmoja huyo sungura mtamuuza kwa tsh 80000/=
ReplyHlw! Natka kujua uhakika wa soko na maeneo ambayo mpo au maeneo ambayo mnaweza kutufikia wateja wenu
ReplyNajaribu kuangalia utofauti wa bei ya kununua sungura wa mbegu, na sungura nitaezalisha mbona hakuna faida, 80,000 kwa elfu 8,000 duuu, tuwe fair basis
ReplyNyie mnatuuzia sungura kwa elfu 80 kisha baadae mnananua kwetu kwa elf 8? hiyo ni sawa kweli?
ReplySuali la Kwanza .
ReplyHivyo vifaav kujengea hilo Banda NI juu yenu au mfugaji.?
Suali la pili.
SUNGURA ananyonyesha kwa muda gani watoto wake ?
Suali la tatu.
Kwa Nini SUNGURA anawivu sana?
Suali la nne.
Kwa Nini SUNGURA anafukia vitoto vyake baada kuzaa? Pia NI muda gani vitoto vinaanza kunyonya na muda gani vinakula majani baada kuzaliwa?
Suali la tano.
Kwanini mnawanyonya wakulima kwa kuwauzia SUNGURA Bei ya juu sana huku nyinyi mkinunua kutoka kwao Bei ndogo kabisa kutoka 80,000 _8,000?