Featured

Latest Update

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI KUFANIKISHA CHANJO BORA

Chanjo mbalimbali za kukinga magonjwa zina utaratibu wake kitaalamu, kama namna ya utunzaji na  namna kuwapa kuku. Zifuatazo ni ...

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI KUFANIKISHA CHANJO BORA

Chanjo mbalimbali za kukinga magonjwa zina utaratibu wake kitaalamu, kama namna ya utunzaji na 
namna kuwapa kuku. Zifuatazo ni dondoo muhimu za kufahamu ili chanjo yako ifanikiwe;
1. Ukihifadhi chanjo yako hovyo hovyo bila kufwata maelekezo ya kitaalamu, chanjo hiyo inakua Sumu 
badala ya kuwa kinga na tiba. Chanjo iliyohifadhiwa vibaya haiwezi kufanikisha matibabu. Chupa za chanjo 
huwa zinakuwa na lebo au karatasi yenye maelekezo ya jinsi ya kutumia pamoja na tarehe ya mwisho ya 
matumizi (Expire date). Usipochanja kuku wako vizuri, ugonjwa unaweza kuenea zaidi.
2. Vifaranga vilivyoanguliwa huweza kuwa na magonjwa mbalimbali yaliyotoka kwa Mama kuku, kupitia 
yai. Kwa hiyo kuwachanja kuku walio na umri chini ya siku kumi (10) ni muhimu sana, kwa sababu itazuia 
magonjwa ambukizi kwa vifaranga kadri wanavyokua.
3. Kila chanjo imetengenezwa kwa kuwekwa mahali sahihi kwenye mwili wa kuku, kuna baadhi huwekwa 
kwenye macho, baadhi kwenye maji na baadhi huchomwa kwa sindano kwenye mabawa. Kwa hiyo 
usibadilishe matumizi ya chanjo.
4. Usiwape chanjo kuku Waliokwisha kuugua [Isipokua kama kuna mlipuko wa ugonjwa wa 
Laryngotracheitis au Fowl pox]
5. Hifadhi chanjo mahali salama pasipokua na joto & mwanga wa jua wa moja kwa moja.
6. Chanjo zilizo nyingi ni viumbe hai visivyoonekana kwa macho (Living micro-organisms) au chembe 
chembe zinazotengeneza magonjwa (disease-producing agents), Kwa hiyo hifadhi chanjo zako kwa 
Uangalifu.
7. Kama unatumia maji ya kunywa kuku kama njia ya kuwapa chanjo, hakikisha Unatumia maji yasiyokua 
na chumvi na Chlorine, kwa sababu chembechembe au viumbe waliopo kwenye chanjo huharibiwa na hizo 
kemikali.
8. Baada ya kutoa chanjo hakikisha unachoma au unavitibu (Kuosha na Kemikali inayoua vimelea vya 
magonjwa, Disinfect) vifaa vyote ulivyotumia wakati wa kutoa chanjo. Ukifanya hivi utazuia kueneza 
magonjwa kwa kuku wazima wasiokua magonjwa.


NG’OMBE WA MAZIWA AINA YA GUERNSEY

Historia

Guernsey ilianzia kwenye Kisiwa kidogo cha Guernsey, kilicho katika Idhaa ya Kiingereza karibu na pwani ya Ufaransa. Hakuna uthibitisho thabiti kuhusu maendeleo ya Guernsey kabla ya Karne ya 19 lakini kunaweza kuwa na ukweli fulani katika nadharia kwamba ng'ombe wa Isigny wa Normandy na aina ya Froment du Léon kutoka Brittany walikuwa jamaa wa mababu wa Guernsey ya kisasa. Kwa kweli, Jersey, Guernsey na Froment du Léon ndio washiriki pekee wa aina ndogo ya ng'ombe wa Kizungu wa Ulaya wa Channel Island.

 Guernsey ilirekodiwa kwa mara ya kwanza kama aina tofauti mnamo 1700. Mnamo 1789, uagizaji wa ng'ombe wa kigeni huko Guernsey ulikatazwa na sheria kudumisha usafi wa kuzaliana ingawa baadhi ya ng'ombe waliohamishwa kutoka Alderney wakati wa Vita vya Kidunia vya pili waliunganishwa na kuzaliana

Ufugaji wa Guernsey ulijenga sifa yake ya uzalishaji wa maziwa bora kutoka kwa nyasi wakati wa karne ya 19 na mapema ya 20 na kisha kusafirisha ng'ombe ili kupata idadi kubwa ya watu katika nchi nyingine kadhaa. Kutoka kwa msingi wa mchanganyiko wa asili, wafugaji wa kisiwa walizingatia kuboresha mifugo kwa kuondoa makosa na kufanya ng'ombe wao kuwa sawa. Yote haya yalitokana na mwonekano wa kuona ulioongezewa na rekodi fulani ya maziwa.

Umashuhuri wa Guernsey kama mzalishaji wa kipekee wa maziwa tajiri ya rangi ya manjano ulimpa jina la "Golden Guernsey".

 

Sifa



Rangi ya Guernsey inatofautiana kutoka njano hadi nyekundu-kahawia na mabaka nyeupe. Wana tabia iliyopangwa vizuri, hawana wasiwasi au hasira. Kimwili kuzaliana hufanana vizuri na ng'ombe wa maziwa na huwasilisha taswira ya mnyama wa kawaida anayefugwa kwa manufaa badala ya mwonekano mzuri. Ng'ombe huyo ana uzito wa kilo 450 hadi 500 kidogo zaidi ya uzito wa wastani wa ng'ombe wa Jersey ambao ni karibu kilo 450 (pauni 1000). Ng'ombe ana uzito wa kilo 600 hadi 700. Wana behewa la kuvutia lenye matembezi ya kupendeza, mgongo wenye nguvu, kiuno mpana, rumbi pana na pipa lenye kina kirefu, kiwele chenye nguvu, kilichoshikamana kinachoenea mbele, na robo zake zikiwa zimesawazishwa na linganifu. Ng'ombe kwa kawaida huingia kwenye maziwa wakiwa na umri wa miaka miwili hivi. Uzito wa wastani wa ngombe na ndama wa kunyonya ni kilo 75. Fahali wa Guernsey ana utu wa kuvutia, akionyesha nguvu na uanaume wa kutosha. Ina mabega ya kuchanganya laini inayoonyesha uboreshaji mzuri, nguvu na hata contour.

FAHAMU(Coccidiosis) Kuhara Damu KWA KUKU DALILI NA JINSI YA KUTIBU

⚠️ Ugonjwa huu Ni ugonjwa unaosababishwa na Protozoa ambao hushambulia kuku na wanyama wengine. 
Ugonjwa huathiri kuku wadogo na wakubwa.

🔺Jinsi Ugonjwa Unavyoenea
🔹 Maambukizi huenea kupitia kinyesi cha kuku wagonjwa kuchafua maji na chakula, udongo na maranda.
🔹 Njia kuu ya maambukizi ni kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa na vimelea
🔹Maambukizi yanaweza pia kupitia vifaa na vyombo vya shambani, nguo, wadudu na wanyama.

🔺Dalili za ugonjwa
🔹Kuhara damu
🔹 Mbawa kushuka 
🔹 Kuzubaa na kuacha kutaga
🔹 Kukosa hamu ya kula
🔹 Kupunguza kasi ya ukuaji na uzito
🔹 Kwa kawaida vifo ni vingi

🔺Uchunguzi wa Mzoga
🔹 Njia ya haja kujaa damu
🔹 Madoa ya damu kwenye utumbo
🔹 Madoa madogo ya rangi nyeupe na nyekundu sehemu ya nje ya utumbo
🔹 Madoa ya rangi ya kijivu sehemu ya ndani ya utumbo
🔹 Utumbo mkubwa mpaka sehemu ya kutolea haja imevimba na kuwa ngumu
🔹 Sehemu ya chini ya utumbo mdogo imevimba na kuwa ngumu
🔹 Utumbo kujaa uchafu wa rangi ya kijivu na kahawia

🔺Tiba ya ugonjwa
🔹 Amprolium hydrochloride/ Esb3 
🔹 Sulfa

🔺Namna ya Kuzuia na Kinga
🔹 Maranda na aina nyingine za malalo yawe makavu wakati wote.
🔹 Fuga kuku kwenye mabanda yenye sakafu isiyo na matundu
🔹 Vyombo vya chakula na maji visiwekwe chini, vining’inie juu ya sakafu kuzuia kuchafuliwa na kinyesi
🔹 Banda lisiwe na msongamano mkubwa wa kuku
🔹 Weka utaratibu wa kuhakikisha wafanyakazi , wageni na ndege hawaingii hovyo kwenye shamba/banda
🔹 Angamiza mizoga yote kwa njia stahiki kwa kuchoma moto au kufukia kwenye shimo refu ardhini. Pia na maranda na vifaa vilivyochafuliwa vichomwe.
🔹 Kutumia dawa za tiba kwa ajili ya kinga. Hii ifanyike kwa muda mfupi kuepuka kuleta usugu wa vimelea.

FAIDA NA UMUHIMU WA VITAMIN KWA KUKU🐓

UKOSEFU  wa VITAMIN kwa Kuku au Upungufu wa VITAMIN hujionyesha kwa namna tofauti katika miili ya kuku, na kila dalili huashiri upungufu wa vitamin.

📌 UMUHIMU WA VITAMINI.
– Husaidia katika ukuaji wa kuku.
– Humfanya kuku muda wote kuwa amechangamka.
– Husaidia kuku kuwa mwenye afya.
– Huwezesha kuku kuwa mtagaji Mzuri.
 
📌 UKOSEFU WA VITAMIN ‘A’ KWA KUKU
Ukosefu wa vtamin ‘A’ hujitokeza baada ya kuku kukosa vyakula vyenye vitamin ‘A’ kwa muda mrefu Kuku wadogo huathirika zaidi kwa kwa ukosefu wa vitamun ‘A’ pia hata kuku wakubwa.
 
📌 DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMIN ‘A’ KWA KUKU
-Macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya mche iliyolowana maji
-Hudhoofika na hatimaye kufa

📌 TIBA NA KINGA
-Kinga ugonjwa huu kwa kuwapa kuku majani mabichi au mchicha au chainizi wakati wa kiangazi au kwa kuku wanaofungiwa ndani na hawawezi kula majani
-Wape kuku vitamini za kuku za dukani wakati majani hayapatikani
-Kwa kuku alie athirika na ugonjwa huu msafishe na maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi hakikisha uchafu wote unatoka kisha mpe vitamin ya dukani… Fanya zoezi hilo kwa siku 5.

 
📌 VITAMINI B
Manyoya huonekana kusambaratika, panga za kuku kuonekana zikiwa zimepauka, na kwa kuku watagaji hupunguza uwezo wao wa kutotoa mayai.
 
📌JINSI YA KUKABILIANA.
Wapatie kuku wako Dawa za multivitamin.
 
📌 VITAMIN E
Hizi ni dalili za ukosefu wa vitamin E kwa kuku,
– shingo huanguka chini na kupinda.
– Vifaranga huanguka kifudi fudi.
– Utagaji wa kuku hushuka kwa kiasi kikubwa.
 
📌 VITAMIN D
Ukosefu wa vitamin D hupelekea tatizo la mifupa kuwa laini, na hali hii hupelekea mifupa kupinda pia magoti huvimba na hata midomo kuwa laini. Na hata ukuaji wa kuku huwa wa hafifu. Hii hutokana madini aina ya madini ya calcium na fosifolusi kutojengeka kwenye mifupa.
Kwa kuku watagaji hali hii hupeleka kwa kuku watagaji kutaga mayai yenye ganda laini.
 
📌JINSI YA KUKABILIANA.
Vitamini hupatikana katika majani mabichi ya mimea, mfano majani ya lusina, mpapai, mchicha na mikunde
Kazi ya vitamini ni kulinda mwili dhidi ya magonjwa, watu wengi hupenda kutumia vitamini mbadala za viwandani kuliko zile vitamini halisia ambayo imetokana na nguvu za jua na madini toka kwenye udongo ambayo hupatikana kwenye majani, ni vyema ukaangalia vitu vinavyopatikana katika eneo lako ili kutengeneza chakula cha mifugo yako

MAMBO 7 YA KUZINGATIA KATIKA ULEAJI WA VIFARANGA

UTANGULIZI
Imekuwa changamoto sana kwa wafugaji wengi. Na mara nyingi kwa wale wanaoanza ufugaji, ufikia hatua hadi kukata tamaa. 

Wakina mama wamekuwa waleaji wazuri sana wa vifaranga. Kwa sababu, wamejifunza tabia ya kuangalia hali ya mtoto wake kila saa. Na vifaranga wanahitaji uangalizi wa hali ya juu sana, ile week ya kwanza.

Leo, natamani ujifunze vitu 7 vya msingi sana katika uleaji wa vifaranga wako.

1. Hakikisha unaweka matandiko safi na salama bandani, urefu wa 5cm. 

2. Hakikisha kuna joto 28’C - 32’C bandani. Kadri vifaranga wanavyokuwa, joto lipunguzwe bandani.

3. Hakikisha kuna hewa safi bandani. Ukiingia bandani hakikisha hamna hewa yenye harufu mbaya

4. Hakikisha kuna mzunguko mzuri wa hewa bandani.

5. Vifaranga wapewe maji safi Na Salama. Vifaranga wanahitajika kunywa maji mengi sana

6. Chakula chenye lishe bora kwa vifaranga.

7. Wiki ya kwanza, hakikisha kuna mwanga muda wote bandani.Vifaranga waweze kula 

Imeandakiwa na #ufugajimakini

UFUGAJI NA UANGALIZI WA KWARE 🐥

*UFUGAJI WA KWARE :*


Sehemu ya Kwanza

Utayarishaji wa banda, Utagaji na uatamiaji mayai, utunzaji vifaranga, uleaji wa vifaranga magonjwa, tiba na kinga.

🔹UTANGULIZI:

Kware ni ndege mdogo mwenye asili ya toka huko Japan. Wakiwa mwituni kware ni ndege wanaohama hama na kuishi mashambani. Rangi ya kware huyu wa mjapan ni yenye madoadoa ya kahawia meupe na meusi yanayoanzia kichwani mwake na hadi mkiani tumboni akiwa na rangi ya kahawia hafi fu. kware pia wanapatikana katika rangi tofauti kama nyeupe tupu, au nyeupe na nyeusi, Kware mkubwa anaweza kuwa na uzito upatao wa gramu 150.

🔹BANDA:

Banda liwe na sifa kama banda la kuku. Kwa kuanza unaweza ukawa na banda la ukubwa wa 1.5m x 1.5m, pia lazima uzingatie usalama
wa vifaranga dhidi ya panya, paka au vicheche. Unatakiwa kuweka ‘magazeti au makasha’ chini kwenye sakafu yatakayosaidia kuondoa hali ya unyevunyevu na pia inakuwa rahisi kulifanyia usafi.

🔹UTAGAJI MAYAI

Wiki ya sita kuelekea ya saba kware wataanza kutaga mayai kila siku. Kwa wastani kware mmoja hutaga mayai 24.

Kware dume humpanda jike kwa muda kidogo, Hapo jike anakuwa tayari kutaga na hutaga mayai 290 hadi 310 kwa mwaka (hii hulingana na lishe nzuri atakayopatiwa).

Mayai ya kware huatamiwa kwa siku 16 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 2, kuanzia siku ya 16 na hadi 18.Njia bora ya kutotolesha mayai ya kware ni kwa kutumia incubator ambapo mayai huatamiwa kwa wingi ndani ya siku 18.


UTUNZAJI WA VIFARANGA

🔹JUMA LA KWANZA

 Vifaranga wapatiwe chakula “Broiler starter” na maji masafi ya kutosha. Siku ya 1 wawekee ‘GLUCOSE’ kwenye maji, Packet moja kwa lita 6 za maji, na siku ya pili hadi ya tano wape vitamini kama vitalyte kwenye maji, siku ya sita wape vitamini pekee kama Stressvita/Farmvita na siku ya saba wapatie chanjo ya Newcastle.

USAFI: Katika juma hili la kwanza chakula kitawekwa chini na tunashauri kuhakikisha vifaranga hawatelezi na kuathiri miguu.

🔺ZINGATIA: Weka goroli au mawe kwenye manywesheo (drinkers) zako ili kuzuia vifaranga wasizame ndani ya (drinkers) maji na kufa.

🔹JUMA LA PILI: 

Vifaranga wataendelea kupewa chakula Broiler starter na maji safi. Wataendelea kuhitaji ‘mwanga’ wa kutosha muda wote na joto la wastani.

🔹JUMA LA TATU

Uhitaji wa joto utapungua, ila ni kipindi ambacho wanakula chakula zaidi kwa ajili ya kukua. Ni vizuri waendelee kupata taa ili kupata mwangaza utakaowawezesha kula mchana na usiku.

🔹SIKU 21 NA KUENDELEA

KWARE wako hawatahitaji joto tena wawekee taa tu za chemli au energy server kipindi cha usiku, wape chakula na maji ya kutosha zaidi kwa ajili ya kukua.


⚠️ MAGONJWA:

KWARE ni ndege wenye kinga kubwa na ni vigumu sana kushambuliwa na magonjwa kama kuku na mara wanapougua ni rahisi sana kutibika. Magonjwa yanayoweza kuwapata kware ni typhoid, mafua na E.Coli.

🔹TIBA KWA KUTUMIA DAWA ZA DUKANI:

Amprolium kwa ugonjwa wa kuharisha damu/ugoro (Coccidiosis), Fluban, Colirid au Doxycol kutibu mafua (Coryza) na Esb3, au Trimazine, Typhoprim, Ancoban hutumika kwa homa ya matumbo (Typhoid).

🔹TIBA MBADALA

Waweza kuwatibu vifaranga au kware wako kwa kutumia tiba mbadala ambayo pia ni rahisi, gharama nafuu na bora zaidi kuliko kutumia madawa yaliyochanganywa na kemikali na yenye gharama. Vifuatavyo ni vitu vya asili vinavyotumika kutibu magonjwa mbali mbali ya kware na yanayopatikana kwa wingi katika maeneo ya mfugaji. Madawa haya hutumika kwa kiwango cha wastani na hayana kipimo maalum kwani hata ukiyazidisha hayana madhara.

🔹MAJANI YA MWAROBAINI

Madawa haya hutumika kutibu kuharisha damu pamoja na mafua kwa vifaranga vya kware Chukua kiasi kidogo cha mwarubaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji yale, kisha weka katika maji uliyoandaa kuwanywesha vifaranga wako. Kata vipande
vidogovidogo vya aloe vera (jani moja laweza kutosha) na tia katika maji yaliyochanganywa na mwarobaini, kisha wapatie vifaranga wanywe (Aloe Vera) itaendelea kujikamua yenyewe ikiwa ndani ya maji huku vifaranga wakiendele kunywa).

🔹KITUNGUU SWAUMU:

Hii hutumika kukinga na kutibu vifaranga vya Kware wanaosumbuliwa na kuharisha damu. Unachukua kitunguu swaumu na kuondoa maganda ya nje kisha kusafi sha na kukata vipande vidogo sana, na kuwawekea kama chakula. Vifaranga wanapenda sana vitunguu hivyo na watakula kwa kasi kama chakula lakini ni tiba tayari. Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapopona.

🔹MAZIWA:

Maziwa yanayotokana na ng’ombe pia hutumika kutibu ugonjwa wa kuhara pamoja na kuwapa nguvu kware waliolegea. Mnyweshe maziwa hayo kware anayeumwa bila kuyachemsha na umnyweshe maziwa ya kutosha kiasi cha kushiba. Unamnywesha mara tatu kwa siku. Hakikisha maziwa unayotumia yanatoka kwa ng’ombe wanaotibiwa kila mara.

⚠️ ANGALIZO:

Siyo lazima kwale waugue ndipo uwapatie tiba hizi. Hakikisha unawapa tiba kabla hata hawajaugua hivyo utawakinga na magonjwa hayo. Waweza kuchanganya madawa hayo yote kwa wakati mmoja kwani hayana madhara.

Endapo madawa ya asili hayapatikani katika eneo la mfugaji basi waweza kuwatibu kwale kwa madawa yafuatayo ambapo vipimo huelezwa moja kwa moja kwa maandishi katika madawa hayo au kuelezwa na muuzaji pale utakaponunulia

🔺CHANJO

Kware wapatiwe chanjo ya “kideri/mdondo” kwa dawa inayoitwa ‘Newcastle’ lasota au T2. Siku ya 7. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Wapewe chanjo ya “gumboro”. inapofi ka Siku ya 14.

Siku ya 21 lazima warudie chanjo ya “Newcastle” na kila baada ya miezi 3 na hakikisha unarudia chanjo ya Newcastle.