Habari ndugu mfugaji, Karibu UFUGAJIMAKINI ufuge kuku kitaalamu,
Ufugajimakini ni Tovuti/Blog ambayo inakupa updates zote za ufugaji wa kuku,
kwa hiyo kama ni mara yako ya kwanza kutembelea blog hii basi usisite kuinakili
na kuchukua taarifa zake za mawasiliano ili wakati mwingine unapohitaji msaada
wa kitaalamu kuhusu ufugaji usiteseke.
Leo ninakuletea Makala hii ya jinsi ya kutiu
kuku wako ugonjwa wa ndui kwa kutumia dawa za asili, ugonjwa wa ndui ni ugonjwa
unaoenezwa kwa virusi.
DALILI ZA UGONJWA WA NDUI.
·
Uonjwa wa ndui utaona kuku wako wamepata
mapele kwenye kichwa yenye rangi ya kahawia, mapele hayo yanaweza kuziba mpaka
macho kufanya kuku wako wasione kabisa na kusababisha kuku wako wakashindwa
kula hivyo wakadhoofika kabisa na hatimaye kufa. Ugonjwa huu huwapata kuku wa
rika zote lakini huathiri sana vifaranga.
Mara nyingi magonjwa ya virusi ni magonjwa
ambayo hayana tiba lakini yana kinga. Wachanje kuku wako hasa vifarnga
wanapokua wamefikia umri wa siku 56
yani wiki nane(8), na kama usipowachanja
kuku wako na kwa bahati mbaya ugonjwa huu ukaingia bandani kwako basi la
kufanya ni hili hapa..
NAMNA YA KUTIBU UGONJWA WA NDUI.
Njia hii nimeshaitumia mara kadhaa pale
ugonjwa ulipowapata kuku wangu na ikanipa matokeo chanya kwa asilimia 95%.
Kwana kabisa nunua OTC 20% pamoja na vitamin, wachanganyie kuku wako kwenye maji ili
kuwaepusha na magonjwa nyemelezi kwa sababu wanpokua wanashambuliwa na ugonjwa
wa ndui ugonjwa wa ndui una sifa ya kupunguza sana kinga ya mwili, kinga ya
mwili kwa kuku wako inashuka sana hivyo inakua rahihisi kwa kuku wako
kuambukizwa magonjwa mengine, kwa hiyo unapokua unawapatia OTC 20% pamoja na VITAMIN
inawasaidia kuboost kinga ya mwili..
Sasa uatafanyaje ili kutibu ugonjwa wa ndui?
Kwanza kabisa tafuta mafuta ya ng’ombe yanapatikana masokoni hasa masoko
makubwa makubwa unaweza ukanunua maziwa freshi ambayo hayajawekewa maji
ukayagandisha alafu ile samli ya juu ukaichukua kama mafuta ya ng’ombe.
Unayafanyaje sasa hayo mafuta ya ngo’mbe,
Mafuta hayo unawapakaa kuku wako maeneo ambayo yana hayo madonda. Unapaka mara
mbili kwa siku asubuhi na jioni ndani ya siku mbili. Baadae yale madonda
yanakua yamelainila na unaweza kuyabandua bila shida yoyota na kuku wako
wanakua vizuri na wanakua wamepona.
kama kuna njia nyingine unayoitumia kutibu ugonjwa huu basi usisite kushare na wengine kwa kucoment hapo chini. Ahsante
19 comments
Write commentstisha mzee baba
ReplyAsante
ReplyAhsante
Replyasante kwa somo zuri, Kadharika unaweza tumia pia mafuta ya kondoo una pakaa kama ulivyo elekeza. itakupatia majibu chanya
ReplyAsate kwa somo njia nyingine in kuwapaka spirit kwenye uvimbe hii inaponesha haraka
Replyyote ni mazuri sana kuna dawa ya asili ya katani unaitwangwa unaipaka kwenye vidonda . magonjwa mengi ya kuku natumia dawa za asili nitafute nikuunge ktk group yetu ya fuga kwa faida no,0755290806
Replykaribu mwanza
ReplyKuku wangu wangu kama wawili au watatu wanakama vidonda vigumu kwenye sikio kwachini ,ila awaonyeshi kuumwa wanachangamka vizuri nakutaga wanataga sielewi sasa iyo imetokana nanini?
ReplyMsaada apo
dawa nyingine ya ndui ni Mtakalang'onyo au Euphorbia, ipo youtube search youtube Tiba za asili za kuku Noah kyando Tv imeelezwa vizur kabisa
ReplyNimeurahi kujua hilo asante mtaalam
ReplyAsante sana
ReplyMm nilijaribu kw kuyabandua mapele na kisha kuwapaka ppf ilosagwa pia sio mbaya
ReplyUko vizuri kaka
ReplyNashukuru sana
ReplyNimejifinza kitu, nashukuru
ReplyNjianjia nyingine ya kutibu ndui ya kuku, chukua maji safii yachemshe kias cha uvuguvugu, maji hayo yachanganye na chumvi kias, safisha kile kidonda kwa kukisugua, mwisho chukua aloevera kata kipande mdondoshee ule ute wa njanonjano unaotoka kwe jani la alovera.. fanya hivyo kwa siku mbili kukuwako atapona vzr
ReplyAsante kwa makala hii nzuri na ya kuelimisha nimejifunza kitu hapo.
ReplyAsante kwa somo
ReplyNa vipi kuhusu jicho kuvimba na kufunga kutoona kabisa
Reply