Featured

Showing posts with label RABITS. Show all posts
Showing posts with label RABITS. Show all posts

MRADI WA UFUGAJI SUNGURA KIBIASHARA.



KIBANDA CHA KUFUGIA
Tunasaidia kwenye ujenzi wa vibanda bora vya sungura,  kwagharama ya Tshs 65,000/=  tu    kwa kimoja cha  ukubwa  wa  futi 2.53  ,  chenye  uwezo  wa  kufugia  Sungura  mmoja  mkubwa  wakuzalisha  pamoja  na watoto wake kwa mwezi mmoja baada yakuzaliwa yaani kipindi chote cha unyonyeshwaji, na kibanda cha saizi hiyo pia kinaweza kufugia hadi sungura kumi wa umri wa miezi mitatu.

Tunashauri ujenzi wa vibanda vitatu kwa kila jike (kupata nafasi ya watoto wanaomaliza kunyonya kwani jike huzaa kila baada ya miezi 2) na pia kibanda kimoja kwa kila dume.

MBEGU
Tunawataka wakulima wetu kufuga mbegu bora na halisi ya sungura watakaotupa nyama bora kwa soko letu,  na  tunawauzia  kwa  gharama  ya  Tshs  80,000/=  kwa  kila  jike  aliyetayari  kubeba  mimba   na  Tshs 40,000/= kwa kila dume mwenye umri wakuzalisha.

MAFUNZO YETU
Tuna  mafunzo  mara  kwa  mara  pia,  na  zaidi  kuhusu  ujezi  wa  mabanda  bora,  Utunzaji  na  ufugaji  kwa ujumla, na kuhusiana na maswala ya magonjwa na namna yakuzuia.
Tuna  saini  mkataba na mkulima/mfugaji  (kwa  ada  maalum  kila  mwaka)  ambao utamuhakikishia mfugaji/mkulima  soko kwa kipindi chote cha mkataba  pale sungura wake wanapokuwa tayari kwa kuuzwa.
Tunanunua sungura katika umri wa miezi 4-5. Kwa umri huo sungura mwenye afya aliyelishwa vizuri anapaswa kuwa na uzito wa kilo 3-4, na kilo moja ya sungura akiwa hai tunamnunua kwa Tshs 8,000/=.


Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

Tafadhali zingatia mafunzo kwa mtunzaji wa sungura wako/au kama ni wewe mwenyewe ni ya muhimu kujifunza mambo ya msingi unapoanza mradi nasi,
Paleunapohitaji ushauri wa kitaalam utagharimia nauli ya mtaalamu atakufundisha UFUGAJI BORA WAKISASA kwa vitendo.

                

UFUGAJI BORA WA SUNGURA


UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu

MABANDA
Kna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.

UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha

2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki
UFUGAJI WA NJE
1 - Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk

2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3 - Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng'oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku

CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates)

USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto

MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12

MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana

UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba

DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo

Baada ya kujua jinsi ya kufuga Sungura kuna watu wanasema ,sungura hawawezi kuliwa? lakini mbona watu wanafanya biashara ya kuuza sungura wa nyama.
wewe unamawazo gani juu ya hii, inalipa?
wasiliana nami..
0759860370