Featured

Ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili): kanuni bora za ufugaji

Dondoo za ufugaji bora wa kuku wa asili

Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi. Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.
 http://ufugajimakini.blogspot.com/
Dondoo ya 1
Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.
2.  Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.
3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.
4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.
5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.
6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.
7.  Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.
Dondoo ya 2
Magonjwa na kinga kwa kuku wote
Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.
Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.
Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.
Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.
Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.
Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.
Dondoo ya 3
Chakula cha ziada
1.  Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.
2.  Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).
3.  Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.
4.  Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.
5.  Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.
6.  Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.
Dondoo ya 4
Utotoleshaji wa vifaranga
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.
Sifa za jogoo bora
1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.
2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.

Sifa za tetea bora
Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.
Uhifadhi wa mayai
1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.
2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.
3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.
4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.
5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.
Kuatamiza mayai
1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.
2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.
3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wilki 2 toka kutagwa.
4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.
5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti
Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja
1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;
2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.
3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.
Dondoo ya 5
Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine
1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasinde mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.
Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.
Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3
Kinga dhidi ya kosidiosisi
Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.
1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.
2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba
3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;
Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho
1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.
2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja
3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.
4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.
5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.
6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.
7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.
8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.
9.  Soma maelezo haya mara kwa mara na ufanye yalioelekezwa.
10.              Washirikishe wengine katika kaya yako ili nao wajifunze na kufanya hivyo kukuza ufugaji na kipato cha familia.


Subscribe to this Blog via Email :

61 comments

Write comments
Unknown
AUTHOR
November 7, 2016 at 10:06 AM delete

naitwa justus me ni mwanafunzi ila natamani sana kufuga kuku lakini mbinu ya kujenga banda la kuku je nifanyeje.naomba ushauri

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
April 17, 2017 at 3:20 PM delete

Habari, nahitaji msaada wa elimu ya ufugaji tafadhali

Reply
avatar
sejna mbaraka
AUTHOR
April 27, 2017 at 4:38 PM delete

Naomba mtu yeyote anaeendesha mradi kama huu anitafute ili niweze kupata elimu zaidi ya kuanza ufugaji nipo chuo kikuu dodoma naombeni sana msaada wenu namba zangu za simu watsap na kawaida
0714077369

Reply
avatar
sejna mbaraka
AUTHOR
April 27, 2017 at 4:43 PM delete

justus kelly habari naona unatatizo kama langu naomba tutafutane tunaweza kushare ideas na kufanikisha ili
namba zangu za simu
0714077369

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
June 17, 2017 at 11:41 AM delete

Nipo dodoma natafuta mbegu nzuri ya kuku wa kienyeji ya tetea na jogoo

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
July 8, 2017 at 2:21 PM delete

Nauza kuku katika mahoteli, mashule,Sherehe, kuku wa kienyeji kutoka singida, Malawi na dodoma napatikana dar es salaam Tanzania. Kwa anae htaj nichek kwa nambie 0718180779

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
August 22, 2017 at 2:40 PM delete

Hata Mimi napenda kufuga sina elim naomba Ali kua tayali no yangu 0745993228

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
September 5, 2017 at 12:23 PM delete

Naomba msaada kwa anayeijua mbegu nzuri ya jogoo na kuku wa kienyeji natak nianze kufuga

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
October 31, 2017 at 8:47 PM delete

ahsante kwa shule nzuri,lakini je nifanyeje ikiwa kuku anataga tu haatamii mapema

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
July 25, 2018 at 1:01 PM delete

Mwenye group la ufugaj wa kuku WhatsApp aniunge namba yangu 0752509718 namim nmeshaanza kufuga kuku wa kienyej

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
September 26, 2018 at 12:53 PM delete

Hello!naomba kuaddiwa katika group la wafugaji namba yangu ni 0756777991

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
November 8, 2018 at 12:59 PM delete

Hello,,me plz 0753 801752 add on watsup

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
November 17, 2018 at 2:06 PM delete

Add me 0737077484 mfugaji makini no utani

Reply
avatar
DJ GERY
AUTHOR
November 18, 2018 at 3:52 AM delete

Add na mm mwexhimiwa 0625728703

Reply
avatar
November 19, 2018 at 5:07 PM delete

Naitwa Billy, mfugaji wa siku,Elimu iliyotolewa bure inatosha,kama unahitaji elimu zaidi waone waganga wa mifugo wapo kila eneo unapoishi ili wakupe elimu na ushauri zaidi, mie natoa natoa elimu na mchoro wa banda la kuku wa kienyeji na jinsi gani utakavyo watunza na uatamiaji nzuri wa mayai. Elimu hiyo utaipata kwa Tsh. 10'000/=

Reply
avatar
November 19, 2018 at 5:08 PM delete

Naitwa Billy, mfugaji wa siku,Elimu iliyotolewa bure inatosha,kama unahitaji elimu zaidi waone waganga wa mifugo wapo kila eneo unapoishi ili wakupe elimu na ushauri zaidi, mie natoa natoa elimu na mchoro wa banda la kuku wa kienyeji na jinsi gani utakavyo watunza na uatamiaji nzuri wa mayai. Elimu hiyo utaipata kwa Tsh. 10'000/= simu yangu +255 753 048 501 / 786 32 46 08

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
January 22, 2019 at 9:10 AM delete

Hell Ndugu na rafiki
Naitwa John
I am from Congo
naomba kuaddiwa katika group la wafugaji namba yangu ni (+243859396987

Reply
avatar
Saibaba
AUTHOR
February 18, 2019 at 11:11 PM delete


Mim naitwa MR sai npo UDOM , nimevutiwa sana na elimu hii likini nilihitaji maelezo zaidi maana hapa naelekea kumaliza na naona fursa pekee ya kunitoa kiuchumi ni hii fursa , na nimeandaa mtaji wa million moja na nuxu, naeweza nisadia pleases nitafte 0683066394 on WhatsApp or normal SMS or call

Reply
avatar
Saibaba
AUTHOR
February 18, 2019 at 11:13 PM delete


Mim naitwa MR sai npo UDOM , nimevutiwa sana na elimu hii likini nilihitaji maelezo zaidi maana hapa naelekea kumaliza na naona fursa pekee ya kunitoa kiuchumi ni hii fursa , na nimeandaa mtaji wa million moja na nuxu, naeweza nisadia pleases nitafte 0683066394 on WhatsApp or normal SMS or call

Reply
avatar
Saibaba
AUTHOR
February 18, 2019 at 11:14 PM delete


Mim naitwa MR sai npo UDOM , nimevutiwa sana na elimu hii likini nilihitaji maelezo zaidi maana hapa naelekea kumaliza na naona fursa pekee ya kunitoa kiuchumi ni hii fursa , na nimeandaa mtaji wa million moja na nuxu, naeweza nisadia pleases nitafte 0683066394 on WhatsApp or normal SMS or call

Reply
avatar
ROSIE MUNISI
AUTHOR
November 22, 2019 at 11:15 AM delete

0717 795182 naomba kuwa added kwa group na mim

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
November 28, 2019 at 9:52 AM delete

Emmanuel nipo mwz, naomba uniunge kwenye group la ufugaji wa kuku wa kienyeji no 0766827778

Reply
avatar
Bilali
AUTHOR
December 6, 2019 at 10:32 AM delete

Naomba nipate elimu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji au kama kuna group la WhatsApp niunge kwa namba 0656300532

Asante

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
January 6, 2020 at 1:10 AM delete

Naomba uniunge ktk group 0621994365

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
January 12, 2020 at 9:17 PM delete

Nashukuru kwa elimu nzuri mtaalamu.kuku wangu Wa kienyeji jogoo ilikuwa amelegea na kashindwa kutembea,nilimchinja nikakuta nyongo imepasuka tumboni kwote kijani tupu.na nyongo ilikuwa kubwa sana.cjajua sababu

Reply
avatar
January 20, 2020 at 2:55 PM delete

Enter your comment...asante kwa elim

Reply
avatar
dj king
AUTHOR
April 2, 2020 at 9:22 AM delete

naomba kuniad kwenye group

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
April 20, 2020 at 12:46 PM delete

Elimu nzuri, ubarikiwe!

Reply
avatar
Mabago
AUTHOR
June 7, 2020 at 11:52 PM delete

Namba yangu ni 0769960894 niadd kwenye group la WhatsApp

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
June 10, 2020 at 12:04 AM delete

0785443304 WhatsApp number

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
June 15, 2020 at 12:49 AM delete

Naomba kuungwa na group la wafungaji wa kuku wa kienyeji ma phone number 0628586360 GOD BLESSING U

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
June 17, 2020 at 9:59 AM delete

0756883521 Pls add

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
June 20, 2020 at 8:26 AM delete

Naomba kwa mtu mwenye kuweza kunipa saport ya kimawazo ndugu yenu kuhusu namna ya kufuga kuku pliz anitafute kupitia namba zifuatazo 0659983950 na kam kunamagroup ya whatsapp naomba ku addiwa

Reply
avatar
Jovith
AUTHOR
June 22, 2020 at 3:18 PM delete

0783065003 plz add me kwenye group

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
August 18, 2020 at 3:01 PM delete

Plz napenda kupata elimu zaid

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
September 23, 2020 at 11:57 AM delete

Nimependa hiyo elimu ya ufugaji wa kuku.naomba kuungwa kwenye group la wafugaji kuku namb yang 0757468673

Reply
avatar
Kutere
AUTHOR
February 7, 2021 at 7:40 PM delete

Habari! Msaada wa kuungwa kwenye grp 0762027375

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
February 21, 2021 at 5:39 PM delete

Naomba uni add kwenye group 0752843486

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
March 6, 2021 at 9:23 AM delete

naomba mniunge na mimi kwenye group la wafugaji wa kuku namba ya yang ya WhatsApp ni 0752960887 na me nataka nianze ufugaji wa kuku kwahyo nahitaji nijifunze zaidi ila niwe na elimu ya kutosha kuhusu ufugaji wa kuku

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
April 6, 2021 at 9:23 AM delete

Naomba link nijiunge kwa group lenu

Reply
avatar
akakorozya
AUTHOR
May 5, 2021 at 3:38 PM delete

Naomba uni add kwenye group 0742 075 214

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
June 29, 2021 at 8:56 AM delete

Nataman xn nfuge kku

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
September 25, 2021 at 3:12 PM delete

Tafadhali kama yupo mwenye whatsap group la ufugaji wa kuku hasa wa kienyeji naomba kuadiwa pia kwa namba 0758387732. Nitashukuru sana

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
January 25, 2022 at 2:00 PM delete

Jaman namm naomba mniad kwenye group namba hyo plZ 0673915902

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
February 25, 2022 at 1:48 PM delete

hongereni sana nimejifunzamamb meng kuhusu ufugaji kuku hasa wa kienyeji

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
April 5, 2022 at 4:02 PM delete

Ahsante Kwa elimu ya ufugaji

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
April 5, 2022 at 4:04 PM delete

Naitwa BENARD magongo nipo dodoma kama kuna group la watsp la ufugaji wa kuku wa kienyeji naombeni mni add Ili niendelee kujifunza zaidi namba yangu ni 0672541876

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
April 29, 2022 at 4:16 PM delete

Kisaka JR nipo mbeya naomba mniadd kwa group la ufugaji wa kuku wa kienyej
+255763 242 879

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
May 15, 2022 at 1:16 AM delete

Dr Andrew. Nipo Tanga nimfugaji chipukizi wa kuku wa kienyeji..muhimu nikujua zaidi kuhusu hao kuku. WhatsApp# 0679972219

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
June 7, 2022 at 2:36 PM delete

Kwa yeyote anaeitaji mbegu za kuku wa kienyeji.
Unaweza kutupata kwa namba ya simu 0684226946 au tembelea ukurasa wetu wa instargram ..familypoultry_tz

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
June 21, 2022 at 3:29 PM delete

Nahitaj elimu zaid kuhus ufugaj

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
June 21, 2022 at 3:38 PM delete

Nomben mni add kweny group la ufugaji kwa no. +255693349130

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
July 20, 2022 at 2:05 PM delete

, muko n'a mafundisho Mazuri Sana, niungge kwenye group WhatsApp ili ni pâte ma funzo zaidi ,+243999529438

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
December 17, 2022 at 7:13 AM delete

Naomba kuungwa kwny group 0718310938

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
January 15, 2023 at 12:28 PM delete

Mimi naitwa Eli niko kigongoni naomba kupata elimu ya ufugaji wa kuku na bata number 0762000984.

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
January 15, 2023 at 12:29 PM delete

whatsapps+255762000984

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
February 7, 2023 at 11:12 AM delete

Please add me whatsapps 0654880904

Reply
avatar
Anonymous
AUTHOR
February 9, 2023 at 8:32 AM delete

Niadd kwenye group la what's app 0685817962

Reply
avatar