Featured

FAHAMU(Coccidiosis) Kuhara Damu KWA KUKU DALILI NA JINSI YA KUTIBU

⚠️ Ugonjwa huu Ni ugonjwa unaosababishwa na Protozoa ambao hushambulia kuku na wanyama wengine. 
Ugonjwa huathiri kuku wadogo na wakubwa.

🔺Jinsi Ugonjwa Unavyoenea
🔹 Maambukizi huenea kupitia kinyesi cha kuku wagonjwa kuchafua maji na chakula, udongo na maranda.
🔹 Njia kuu ya maambukizi ni kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa na vimelea
🔹Maambukizi yanaweza pia kupitia vifaa na vyombo vya shambani, nguo, wadudu na wanyama.

🔺Dalili za ugonjwa
🔹Kuhara damu
🔹 Mbawa kushuka 
🔹 Kuzubaa na kuacha kutaga
🔹 Kukosa hamu ya kula
🔹 Kupunguza kasi ya ukuaji na uzito
🔹 Kwa kawaida vifo ni vingi

🔺Uchunguzi wa Mzoga
🔹 Njia ya haja kujaa damu
🔹 Madoa ya damu kwenye utumbo
🔹 Madoa madogo ya rangi nyeupe na nyekundu sehemu ya nje ya utumbo
🔹 Madoa ya rangi ya kijivu sehemu ya ndani ya utumbo
🔹 Utumbo mkubwa mpaka sehemu ya kutolea haja imevimba na kuwa ngumu
🔹 Sehemu ya chini ya utumbo mdogo imevimba na kuwa ngumu
🔹 Utumbo kujaa uchafu wa rangi ya kijivu na kahawia

🔺Tiba ya ugonjwa
🔹 Amprolium hydrochloride/ Esb3 
🔹 Sulfa

🔺Namna ya Kuzuia na Kinga
🔹 Maranda na aina nyingine za malalo yawe makavu wakati wote.
🔹 Fuga kuku kwenye mabanda yenye sakafu isiyo na matundu
🔹 Vyombo vya chakula na maji visiwekwe chini, vining’inie juu ya sakafu kuzuia kuchafuliwa na kinyesi
🔹 Banda lisiwe na msongamano mkubwa wa kuku
🔹 Weka utaratibu wa kuhakikisha wafanyakazi , wageni na ndege hawaingii hovyo kwenye shamba/banda
🔹 Angamiza mizoga yote kwa njia stahiki kwa kuchoma moto au kufukia kwenye shimo refu ardhini. Pia na maranda na vifaa vilivyochafuliwa vichomwe.
🔹 Kutumia dawa za tiba kwa ajili ya kinga. Hii ifanyike kwa muda mfupi kuepuka kuleta usugu wa vimelea.

Subscribe to this Blog via Email :