Watu wengi hapa nchini hujihusisha na ufugaji wa kuku kwa lengo la kujipatia chakula na kipato. Mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku ni pamoja na mayai, nyama, mbolea na manyoya kwa matumizi mbalimbali. Mifumo ya ufugaji kuku ambayo hutumika hapa nchini ni huria, nusu huria na shadidi. Ufugaji wa kuku utakuwa endelevu na wenye tija kwa kufuata kanuni za ufugaji bora zifuatazo:-
• Kufuga kuku kwenye banda bora,
• Kuchagua kuku bora wa kufuga,
• Kutunza na kulisha kuku kulingana
na hatua mbalimbali za ukuaji
• Kudhibiti na kutibu magonjwa ya
kuku
• Kutunza kumbukumbu.
1 Banda la Kuku
Kuku
huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Banda bora la kuku
linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
• Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi
kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi
na mvua pamoja na wanyama hatari,
• Lenye mwanga, hewa na nafasi ya
kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa
urahisi,
• Lijengwe sehemu yenye mwinuko
isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi
watu,
• Liwe na vichanja kwa ajili ya
kuku kupumzika na kulala
• Liwe na sehemu ya kuwekea
chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga,
• Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya
kuku na kuweka vyombo vya chakula na
maji,
• Kwenye mazingira ya joto banda
liwe la ukuta mfupi na sehemu ya kubwa
wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa
• Kwenye mazingira ya baridi banda
liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili
kupitishia hewa na mwanga.
1.1 Vifaa Vinavyotumika kwa
Ujenzi wa Banda
Vifaa
vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika.
Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-
• Sakafu -
Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
• Kuta -
Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi, udongo, matofali, mawe, mabati na
wavu
• Paa -
Nyasi, makuti, majani ya migomba,
mabati na vigae.
• Wigo -
Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi,
mianzi,matete, wavu na mabati
1.2 Ukubwa wa Banda
Ukubwa
wa banda utategemea idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku. Kuku wanahitaji
nafasi tofauti kutegemea umri, aina na njia ya ufugaji. Eneo la mita moja ya
mraba linatosha kwa vifaranga 16 wa umri wa wiki 1 – 4. Hivyo banda lenye mita
za mradi 16 linaweza kulea vifaranga 320 hadi wiki 4. Baada ya wiki 4 eneo hili
liongezwe kutegemea aina ya kuku na njia
inayotumika katika ufugaji kama inavyoonekana kwenye jedwali Na. 10
Jedwali Na 10: Eneo Linalohitajika Kufuga Kuku Kwenye Sakafu ya Matandazo Kutegemea na Umri na Aina ya Kuku
Umri wa
Kuku
|
Idadi
ya Kuku kwa mita 1 ya mraba
|
|
Kuku wa
mayai
|
Kuku wa
nyama
|
|
Siku 1
hadi wiki 4
|
18
|
18
|
Wiki ya
5 hadi ya 8
|
9
|
9
|
Wiki ya
9 hadi 20
|
6
|
-
|
Wiki
21 kuendelea
|
3-4
|
-
|
Angalizo:
Mabanda
yanayozungushiwa wigo kama ilivyo katika mfumo wa nusu huria, kuku mmoja
huhitaji eneo la wazi lenye ukubwa wa mita za mraba 10. Mfano, kuku 100 huhitaji eneo la mita za mraba 1000
1.3 Vifaa na Vyombo Muhimu
Mfugaji
anashauriwa kutumia vifaa na vyombo maalum ili kurahisisha na kuboresha utunzaji wa makundi mbalimbali ya kuku. Vifaa
na vyombo vinavyohitajika kwa ajili ya kuwekea chakula na maji, kutagia mayai
na kupumzika vinapatikana kwenye maduka ya pembejeo za mifugo. Aidha, mfugaji
anaweza kutengeneza mwenyewe kwa kutumia malighafi zilizopo kwenye mazingira
yake.
2
Uchaguzi
wa Kuku Bora wa Kufuga
2.1
Kuku
wa Asili
Aina za kuku wa asili wanaopatikana hapa nchini ni pamaja na Kuchi (Kuza),
pori (Kishingo), Njachama, Kinyavu,
Mbuni na Tongwe (Msumbiji). Mfugaji anaweza kuongeza uzalishaji kwa kuchagua kuku mwenye sifa
zifuatazo:-
• Uwezo wa kutaga mayai mengi (kati ya 15-200 katika mzunguko
mmoja wa utagaji (Jedwali Na 11),
• Uwezo wa kuatamia na kuangua
vifaranga wengi, • Uwezo wa kustahimili magonjwa
• Umbo kubwa na kukua haraka.
Jedwali
Na 11: Masuala ya Kuzingatia Wakati wa Kumchagua Kuku Mtagaji Asili
Viungo
vya mwili
|
Sifa
|
Macho
|
Maangavu,
yenye wekundu kwa mbali na makubwa yamejaa kwenye soketi za macho.
|
Mdomo
|
Wenye
rangi ya njano kwa mbali
|
Kisunzu/Upanga
|
Chekundu, Laini,kimelala kidogo
upande na kinang’aa
|
Shingo
|
Iliyosimama
|
Umbali
kati ya kidali na nyonga
|
Upanga
wa vidole 3-4 vya mpimaji
|
Upanga
wa nyonga
|
Upana
wa vidole 3 vya mpimaji
|
2.2
Kuku
wa Kisasa
Kuku
bora wa kisasa kwa ajili ya mayai au
nyama ni mwenye sifa zifuatazo:-
• Uwezo wa kuanza kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 5-6) kutegemea na
koo,
• Umbo kubwa na anayekula haraka (kilo 1.5-2.0 kwa
kipindi cha wiki 8-120 kutegemea na koo kwa kuku wa nyama,
• Anayetaga mayai mengi (250 au
zaidi) kwa kuku wa mayai kwa mwaka; na
• Awe na uwezo wa kutaga katika
umri wa miezi 6-8.
2.3
Uchaguzi
wa Jogoo Bora wa Mbegu
Jogoo wa mbegu anatakiwa awe na
sifa zifuatazo:-
•
Achaguliwe
kutoka kwenye koo zenye sifa ya kutaga mayai mengi,
• Mrefu, umbo kubwa, miguu imara na
yenye nguvu,
• Awe machachari, ushawishi kwa
mitetea na ari ya kupanda
• Uwezo wa kupanda akiwa na umri wa
miezi 7-10.
3 Mayai kwa Ajili ya Kutotoa Vifaranga
3.1 Uchaguzi wa Mayai
Mayai kwa ajili ya kutotoa
vifaranga yawe na sifa zifuatazo:-
• Yaliyorutubishwa na jogoo,
• Yasiwe na nyufa,
• Yasiwe na maganda tepetepe,
• Yasiwe na kiini kilichovunjika,
• Yawe na ukubwa wa wastani; na
• Yasiwe yamekaa zaidi ya wiki 2
baada ya kutagwa.
3.2 Utunzaji wa Mayai
Mayai ya
kienyeji kwa ajili ya kutotoa vifaranga yatunzwe kwa kusimamishwa wima sehemu
iliyochongoka ikiwa imeangalia chini kwa siku 3 za mwanzo na kisha yageuzwe ili
sehemu iliyobutu iangalie chini. Mayai yahifadhiwe kwenye sehemu iliyo na
ubaridi kidogo na giza.
4. Utunzaji wa Kuku kwa Makundi
1. Utunzaji wa Vifaranga
Malezi
bora ya vifaranga ni muhimu katika ufugaji wa kuku kwa sababu vifaranga hawana uwezo wa kustahimili
mazingira wakiwa wenyewe mara wanapoanguliwa.Ukosefu wa malezi bora husababisha vifaranga kuwa dhaifu,kufa kwa
wingi na hivyo kupunguza idadi ya kuku wa baadaye. Malezi ya vifaranga yanaweza
kufanyika kwa kutumia kuku walezi au kutumia vifaa maalum.
Kulea Vifaranga kwa Kutumia Kuku Mlezi
Vifaranga wanaweza kulelewa na mama yao au
kuku mlezi. Endapo kuku wengi wametotoa vifaranga kwa wakati mmoja, achaguliwe
kuku mlezi aliye na uwezo wa kulea vifaranga wengi kati ya waliototoa aendelee kulea na wengine
waliototoa waachwe huru ili warudi kwenye mzunguko wa kutaga. Kuku mmoja
anaweza kulea vifaranga 20 hadi 25. Mfugaji wa kuku,pamoja na kanuni nyingine,
anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
• Kuku anayelea vifaranga atengewe
chumba maalumu, apewe maji ya kutosha na chakula chenye virutubisho muhimu,
• Vifaranga wasiachiwe kutoka nje
hadi watakapofika umri wa wiki 6,
• Vifaranga watengwe na mama/mlezi
baada ya wiki 4 kuruhusu mama aendelee na mzunguko wa kutaga;na
• Katika maeneo yenye hali ya hewa
ya ubaridi vifaranga wacheleweshwe kutenganishwa na mama/mlezi hadi wiki ya 6 au
mpaka waonekane wameota
manyoya ya kutosha
Kulea Vifaranga kwa Kutumia Bruda
Bruda ni chombo/sehemu iliyoandaliwa mahusus
kwa ajili ya kuwapatia joto vifaranga badala ya mama/mlezi. Mfugaji anaweza
kulea vifaranga wengi kwa kutumia bruda ambayo ni mduara unaweza kutengenezwa
kwa kutumia mbao, karatasi ngumu au kwa kuziba pembe za chumba.Aidha, njia hii
hupunguza vifo vya vifaranga vinavyosababishwa na ndege au wanyama
hatari,huruhusu kuku kutaga mapema zaidi na kuwa na mizunguko mingi ya utagaji
(kwa kuku wanaoatamia). Vilevile, hurahisisha udhibiti wa magonjwa.
Mfugaji
anapaswa kufuata taratibu zifuatazo katika kulea vifaranga kwa kutumia bruda:-
• Kuweka vifaa vya kuongeza joto
kwa mfano taa ya umeme, chemli au jiko la mkaa. Zingatia kiwango cha joto
kinachohitajika katika bruda.
Wiki ya kwanza ni 35oc, wiki ya pili ni 33oc,
wiki ya tatu ni 31oc na wiki ya nne
ni 29oc,
• Kuchunguza mtawanyiko wa
vifaranga ndani ya bruda ili kutathimini hali ya joto.Wakijikusanya kwenye
chanzo cha joto, inaashiria kuwa baridi imezidi hivyo joto liongezwe. Wakiwa
mbali na chanzo cha joto maana yake joto limezidi hivyo joto lipunguzwe,
• Bruda iwe na sakafu yenye malalo
yatokanayo na maranda ya mbao au pumba za mpunga. Malalo yabadilishwe endapo
yataonekana yameloana,
• Bruda iwekwe vifaa vya maji na chakula. Maji na
chakula kiwekwe kabla ya kuweka vifaranga,
• Vifaa vya joto viwekwe ndani ya
bruda masaa 6 kabla ya kuingiza vifaranga,
• Vifaranga walishwe chakula cha
kuanzia gramu 12-15 kwa kipindi cha wiki ya 2. Katika wiki ya 3 wapewe gramu
21-35 kwa kifaranga na chakula hicho kiwepo muda wote,
• Vifaranga wapatiwe vitamin,
madini na dawa za kinga (antibiotics); na
• Vifaranga wapatiwe chanjo
kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa mifugo.Chanjo dhidi ya magonjwa muhimu
kwa mfano,Marek’s (mara anapototolewa), Mdondo (siku ya 3-4 na kurudiwa baada
ya siku ya 21 na kila baada ya miezi 3) na Gumboro (siku ya 7na kurudia tena
siku ya 21).Wapatiwa dawa ya minyoo (wiki ya 8) na coccidiosis(wiki ya 3-4).
Siku ya 45 wapewe chanjo ya ndui ya kuku.
2. Kutunza Kuku Wanaokua (Wiki 8-18)
Utunzaji wa kundi hili unategemea mfumo
unaotumika.
Kuku Wanaofugwa Katika Mfumo Huria
Kuku wanaofugwa katika mfumo huu wapatiwe matunzo
bora yakiwemo yafuatayo;
• Wapewe chakula cha ziada asubuhi
kabla ya kutoka na wanaporudi kwenye banda. Chakula hicho kinaweza
kugawanywa mara ya 2 kwa siku,
• Wapatiwe maji safi na ya kutosha
wakati wote
• Wapatiwe chanjo na dawa kulingana
na ushauri wa mtaalam wa mifugo. Wiki ya kumi warudie chanjo ya mdondo, wiki ya
12 kuhara (fowl cholera), wiki ya 14 ndui ya kuku,
Kuku Wanaofugwa Katika Mfumo Shadidi
• Majogoo watenganishwe na mitetea
katika wiki 7 hadi 10 ili kuzuia
uzaliano usio na mpangilio,
• Wapewe chakula cha kukuzia
kuanzia wiki ya 8-15 gramu 55-60 na kuanzia wiki ya 16 gramu 65-80 kwa
wanaofugwa mfumo huria na gram 120-125 kwa kuku kwa siku kwa wanaofugwa mfumo
wa shadidi,
• Kuku wa nyama wapatiwe chakula
cha kuku wa nyama muda wote,
• Wapatiwe maji safi ya kunywa kwa muda wote kwenye vyombo safi,
• Kuku wachunguzwe dalili zozote za
ugonjwa ili waweze kupata tiba sahihi kutoka kwa mtalaamu wa mifugo,
• Kuku wa wiki 9-20 wanahitaji
nafasi ya mita za mraba 0.15 kwa kuku na wiki 21 au zaidi mita za mraba 0.2 kwa
kuku,
• Kuwe na vyombo maalum vya kutosha
kwa ajili ya chakula na maji,
• Wafanyiwe usafi wa banda mara kwa
mara ili kuzuia magonjwa yanayotokana na uchafu
• Wakatwe midomo ili kuzuia
kudonoana.
3. Kuku Wanaotaga
Mahitaji ya kuku wanaotaga ni tofauti na
makundi mengine.
Mambo ya kuzingatia kwa kuku
wanaotaga ni pamoja na:-
• Banda liwe na viota vya kutagia
mayai (kiota 1 kwa kuku 3-5).Viota viwekwe bandani mara kuku
watakapofikisha umri wa wiki 18 ili
waanze kuzoea kuvitumia,
• Wapatiwe chakula na maji safi
wakati wote kwa kutumia vyombo maalum ambavyo ni visafi,
• Kuku wasiotaga waondolewe kwenye kundi.Kuku hao
huonekana wasafi na sehemu ya kutolea yai huwa ndogo na kavu,upanga wake kichwa
(comb) huwa mdogo na mwekundu,
• Wapatiwe dawa ya minyoo kila
baada ya miezi 3,
• Wawekewe fito au ubao mwembamba
kama sehemu ya kupumzikia na mazoezi ili kuzuia kudonoana,
• Mayai yakusanywe mara 4 au zaidi
kwa siku ili yasidonolewe na kuku,
• Kuwe na malalo makavu na
yabadilishwe mara yanapochafuka,
• Vyombo vifanyiwe usafi kila ili
kuzuia magonjwa; na
• Watundikiwe majani mabichi aina
ya mchicha,papai, alfaafa,majani jamii ya mikunde ili kuboresha lishe.
Udhibiti na Tiba Dhidi ya Magonjwa ya Kuku
Kuku wanaopata lishe bora, kutunzwa vizuri na kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa
yanayotokea mara kwa mara huwa na afya
nzuri. Ni bora kuzuia magonjwa kuliko kutibu ili kupunguza vifo na gharama.
Iwapo ugonjwa utatokea kuku wagonjwa watenganishwe na kuku wasio wagonjwa na wapatiwe tiba.
Kanuni muhimu za kufuata ili kuzuia magonjwa ni:-
• Banda liwe safi muda wote,
• Kabla ya kuweka kuku, banda linyunyuziwe
dawa ya kuua wadau wa magonjwa mbalimbali,
• Kuku wakaguliwe kila siku ili
kubaini wagonjwa au wenye matatizo, kuwatenga na kutoa taarifa kwa mtaalam wa mifugo,
• Kuku wapatiwe chanjo dhidi ya
magonjwa mbalimbali,
• Watu wasiohusika wasiingie eneo
la kufugia kuku bila utaratibu,
• Ndege na wanyama wengine wasifike
eneo la kufugia kuku,
• Banda la kufugia kuku
litenganishwe na mabanda ya mifugo mingine,
•
Lango
la kuingia katika banda la kuku liwekewe dawa ya kukanyaga kwa wanaoingia ndani
ili kuzuia kuingiza vimelea vya wadudu wa magonjwa;na
• Vifaa vya chakula na maji viwe
safi wakati wote.
Dalili za Kuku Mgonjwa
Dalili za ujumla zinazoonekana kwa kuku
mgonjwa ni kama zifuatazo:-
• Kuzubaa,
• Kupoteza hamu ya kula,
• Kujitenga na wenzake katika
kundi; na
• Kupunguza au kusimama kutaga.
Mfugaji anapoona mojawapo ya dalili hizo
atoe taarifa kwa mtaalum wa mifugo
Ufugaji wa Aina Nyingine za Ndege
Aina ya ndege wengine wanaofugwa hapa nchini
ni pamoja na Bata maji,Bata bukini, Bata bukini, Kanga na Njiwa. Ndege hao
hufugwa kwa kiasi kidogo ukilinganishwa na kuku kwa kuwa soko lao ni
dogo.Utunzaji wao hautofautiani sana na kuku;
• Wajengewe banda la kuishi ambalo
ukubwa wake utagemea idadi ya ndege wanaofugwa,
• Wapatiwe chakula chenye
virutubisho na maji ya kunywa yakutosha,
• Wapatiwe kinga na tiba dhidi ya
magonjwa,
• Bata maji na Bata bukini
wajengewe bwawa lenye nafasi ya kukutosha kwa ajili ya kuogelea; na
• Njiwa wajengewe viota sehemu ya
juu kama kwenye mapaa ya nyumba.
Utunzaji wa Kumbukumbu
Utunzaji
wa kumbukumbu ni muhimu sana katika ufugaji wa kuku na ndege wengine wafugwao
ili kusaidia mfugaji kujua maendeleo ya ufugaji wake. Utaratibu wa kuweka
kumbukumbu mara tukio linapotokea ni lazima ili kuepuka kusahau.Mfugaji
ahakikishe anaweka kumbukumbu ambazo ni sahihi na zinazoeleweka.
Aina za Kumbukumbu
Kumbukumbu zinazopaswa kuwekwa ni pamoja
na:-
• Aina na idadi ya kuku waliopo
kwenye kila kundi (mfano vifaranga,wanaokua,wanaotaga,majogoo),
• Uzalishaji wa mayai kwa kundi la
kuku waliopo,
• Utotoaji wa vifaranga,
• Kinga na matibabu,
• Mapato na matumizi,
• Utagaji wa kila kuku na utunzaji
(kwa kuku wa asili); na
• Kumbukumbu za vifo.
Chakula na uchanganyaji wake
Chakula
ndicho huchangia sana katika gharama za uzalishaji kwa zaidi ya asilimia 60. Na
gharama ya chakula huongezeka kila mwaka kuliko hata gharama za mayai au kuku
wenyewe.
Mfugaji
anaweza kununua chakula kilichochanganywa au kuchanganya mwenyewe. Ila anapaswa
kuzingatia virutubisho na viini lishe vilivyopo katika chakula hicho pia
kuzingatia mahitaji ya kuku wake.
Virutubisho
vinavyotakiwa ni vingi lakini vimegawanywa katika makundi sita ya vyakula
ambavyo ni; protin, wanga, mafuta, madini,vitamini na maji.
Protini
inahitajika kujenga mwili wa kuku. Ni muhimu kwa ukuaji wa kuku, uzalishaji wa
mayai na kuimarisha afya. Wanga na mafuta vinahitajika ili kuupa mwili nguvu na
joto na kuwezesha mwili kufanya kazi zake ipasavyo. Vitamini vinahitajika ili
kumwezesha mwili wa kuku kufanya kazi zake vizuri. Madini yanahitajika ili
kuimarisha mifupa na uzalishaji.
Uchanganyaji
wa chakula
Vyakula
|
Vifaranga
Nyama
|
Nyama
kuzia
|
Vifaranga
Mayai
|
Mayai
Kuzia
|
Mayai
Taga
|
Ng’ombe
maziwa
|
Mahindi
|
38
|
28
|
28
|
26
|
20
|
0
|
Pumba
mahindi
|
19
|
26
|
24
|
30
|
30
|
40
|
Pumba
mpunga
|
15
|
18
|
24
|
25
|
30
|
33
|
Mashudu
alizeti
|
8
|
8
|
6
|
5
|
6
|
15
|
Soya
|
4
|
6
|
6
|
5
|
6
|
5
|
Dagaa
|
10
|
7
|
5
|
3
|
3
|
0
|
Damu
|
4
|
5
|
4
|
3
|
2
|
0
|
Chokaa
mifugo
|
1
|
1
|
2
|
2
|
2
|
5
|
Madini
|
0.5
|
0.5
|
0.5
|
0.5
|
0.5
|
1.5
|
Chumvi
|
0.5
|
0.5
|
0.5
|
0.5
|
0.5
|
0.5
|
Jumla
|
100
|
100
|
100
|
100
|
100
|
100
|