Nguruwe ni mnyama mwenye faida, ni
rafiki kwa mazingira na hahitaji gharama kubwa
“Ufugaji wa Nguruwe ni lazima uwe wa
kisasa ili kupata mazao bora. Unaweza kupata kila unachohitaji wewe, familia na
hata ndugu zako kutokana na ufugaji wa nguruwe”, anasema Bwana Lomaiyani Molel
kutoka Arusha. Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu
na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake
inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama
nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya
kipindi cha miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo.
Ufugaji
Kwa kawaida nguruwe wanafugwa na watu wa kada zote, wafugaji wadogo wadogo na hata wakubwa. Aina hii ya ufugaji huweza kumpatia mkulima kipato pamoja na lishe kwa familia, na hauhitaji gharama kubwa.
Banda
Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa vifaa nafuu. Unaweza kutumia mchanga na simenti kuweka sakafu, ama ukatumia udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kuweka sakafu. Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka guruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja.
Malisho
Ulishaji wa nguruwe ni rahisi kwa kuwa wanakula aina mbalimbali za vyakula kulingana na mazingira wanayofugwa. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali, na pia hulishwa kwa kutumia masalia ya nafaka (pumba). Unaweza kuwalisha kwa kutumia mashudu au pumba aina ya Wheat Poland. Pia unaweza kuwalisha kwa kutumia mabaki ya jikoni.
Kuzaliana
Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114, ambazo hugawanyika kwa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Nguruwe mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 6 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 8 wanakuwa na uzito kati ya kilo 50-70 na wanaweza kuuzwa.
Matunzo
Baada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili.
MAGONJWA YANAYOATHIRI NGURUWE
Kuna aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia nguruwe, lakini yapo yale yaliyozoeleka ambapo ni lazima kukabiliana nayo ili kuwa na ufugaji wenye tija.
1. Ugonjwa wa miguu na midomo
Ugonjwa huu huathiri nguruwe sehemu za miguu na midomo. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.

Chanjo: Chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa midomo na miguu (FMD vaccine) hutolewa kila baada ya mwaka mmoja. Hii inasaidia kuwaweka nguruwe wako katika hali nzuri zaidi bila kushambuliwa na magonjwa hayo.
Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.
2. Homa ya Nguruwe (Swine fever)
Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa
ya nguruwe huenea kwa haraka sana miongoni mwa makundi ya nguruwe,
na huua kwa haraka sana, lakini hauna madhara kwa binadamu na
hauambukizwi kwa binadamu. Nguruwe walioambukizwa waanshikwa na
vindonda ama mapunye kwenye ngozi. Pia masikio na ngozi huwa
mekundu.
Chanjo:
Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa
salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza
kuteketeza kwa kuwachoma moto.
Muhimu:
Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana
ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya
kuweka nguruwe wengine.
3. Ugonjwa wa mapafu (Pneumonia)
Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, ambapo husababisha kukohoa na kupumua kwa shida. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.
Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.
4. Kimeta (Anthrax)
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi.
Chanjo: Chanja nguruwe wako dhidi ya kimeta kama utakavyoelekezwa na wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.
Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.
Muhimu: Homa ya nguruwe ni lazima iwekewe karatini kwa sababu husambaa kwa haraka sana. Nchini Tanzania mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukitokea mara kwa mara maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Malawi na katika mkoa wa Mbeya.

2 comments
Write commentsNATAKA KUPATA FAIDA KWA HARAKA JE,NIFANYEJE?
ReplyKunya
Reply