Featured

MRADI WA UFUGAJI SUNGURA KIBIASHARA.



KIBANDA CHA KUFUGIA
Tunasaidia kwenye ujenzi wa vibanda bora vya sungura,  kwagharama ya Tshs 65,000/=  tu    kwa kimoja cha  ukubwa  wa  futi 2.53  ,  chenye  uwezo  wa  kufugia  Sungura  mmoja  mkubwa  wakuzalisha  pamoja  na watoto wake kwa mwezi mmoja baada yakuzaliwa yaani kipindi chote cha unyonyeshwaji, na kibanda cha saizi hiyo pia kinaweza kufugia hadi sungura kumi wa umri wa miezi mitatu.

Tunashauri ujenzi wa vibanda vitatu kwa kila jike (kupata nafasi ya watoto wanaomaliza kunyonya kwani jike huzaa kila baada ya miezi 2) na pia kibanda kimoja kwa kila dume.

MBEGU
Tunawataka wakulima wetu kufuga mbegu bora na halisi ya sungura watakaotupa nyama bora kwa soko letu,  na  tunawauzia  kwa  gharama  ya  Tshs  80,000/=  kwa  kila  jike  aliyetayari  kubeba  mimba   na  Tshs 40,000/= kwa kila dume mwenye umri wakuzalisha.

MAFUNZO YETU
Tuna  mafunzo  mara  kwa  mara  pia,  na  zaidi  kuhusu  ujezi  wa  mabanda  bora,  Utunzaji  na  ufugaji  kwa ujumla, na kuhusiana na maswala ya magonjwa na namna yakuzuia.
Tuna  saini  mkataba na mkulima/mfugaji  (kwa  ada  maalum  kila  mwaka)  ambao utamuhakikishia mfugaji/mkulima  soko kwa kipindi chote cha mkataba  pale sungura wake wanapokuwa tayari kwa kuuzwa.
Tunanunua sungura katika umri wa miezi 4-5. Kwa umri huo sungura mwenye afya aliyelishwa vizuri anapaswa kuwa na uzito wa kilo 3-4, na kilo moja ya sungura akiwa hai tunamnunua kwa Tshs 8,000/=.


Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

Tafadhali zingatia mafunzo kwa mtunzaji wa sungura wako/au kama ni wewe mwenyewe ni ya muhimu kujifunza mambo ya msingi unapoanza mradi nasi,
Paleunapohitaji ushauri wa kitaalam utagharimia nauli ya mtaalamu atakufundisha UFUGAJI BORA WAKISASA kwa vitendo.

                

Subscribe to this Blog via Email :

18 comments

Write comments
Unknown
AUTHOR
July 4, 2018 at 3:03 PM delete

Sijambo doctor ninahitaji kufuga Ila nipo Dodoma inawezekana

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
August 17, 2018 at 10:57 AM delete

habar dr. naitwa rashidi nipo dodoma nahitaji kufuga sungura kibishar nmaweza pata muongozo wako please

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
May 24, 2019 at 10:34 AM delete

Naweza pata msfunma zaidi

Reply
avatar
KISINZI
AUTHOR
June 5, 2019 at 9:16 PM delete

Niko Morogoro Ifakara. Je ninaweza kupata nafasi kwa mafunzo ya mwangalizi wa sungura halafu ninunue majike? 0784453115

Reply
avatar
KISINZI
AUTHOR
June 5, 2019 at 9:17 PM delete

Niko Morogoro Ifakara. Je ninaweza kupata nafasi kwa mafunzo ya mwangalizi wa sungura halafu ninunue majike? 0784453115

Reply
avatar
Max
AUTHOR
June 26, 2019 at 6:56 PM delete

Doctor nngependaa kupata mawasiliano na ww binafsi namba zangu n 0678278404 na pia email yangu n Bboymax129@gmail.com ningependaa tuwasiliane naitwa max namengi yakuzungumzaa mtaalamu

Reply
avatar
Gamson
AUTHOR
July 29, 2019 at 11:50 AM delete

habari daktari nipo mlandizi na ningependa kuanza rasmi ufugaji wa sungura kibiashara naomba mwongozo.Anuani pepe ni ahimidiwe@gmail.com

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
November 1, 2019 at 11:12 AM delete

nyie mnaniuzia sungura kwa 80,000 halafu mie sungura huyo nakuuzia wewe kwa kilo 8000 akiwa na kilo 4 unamnunua 32000, mimi namkuza mpaka anafikia umri wa miezi 4 inamaana huyo sungura atakuwa na muda mfupi wa kushika mimba, mimi mkulima nafaidikaje?

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
February 18, 2020 at 3:03 PM delete

Habari mtaalamu. Naomba namba zako za simu. Napatikana kwa pkilasara@yahoo.co.uk

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
April 12, 2020 at 12:32 PM delete

Naomba michoro ya banda LA sungura, nitanunua sungura Wa kuanzia.

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
May 6, 2020 at 10:06 PM delete

Jaribuni kutokumnyonya sana mkulima.... Angalau kila moja iwe 12000/= maana nyie baada ya mwezi mmoja huyo sungura mtamuuza kwa tsh 80000/=

Reply
avatar
May 14, 2020 at 9:43 PM delete

Hi nipo Dom nahitaji kuanza mradi

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
May 16, 2020 at 11:36 AM delete

Hlw! Natka kujua uhakika wa soko na maeneo ambayo mpo au maeneo ambayo mnaweza kutufikia wateja wenu

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
July 29, 2020 at 1:39 PM delete

Najaribu kuangalia utofauti wa bei ya kununua sungura wa mbegu, na sungura nitaezalisha mbona hakuna faida, 80,000 kwa elfu 8,000 duuu, tuwe fair basis

Reply
avatar
Wambura
AUTHOR
October 12, 2020 at 7:26 PM delete This comment has been removed by the author.
avatar
Wambura
AUTHOR
October 12, 2020 at 7:27 PM delete

Nyie mnatuuzia sungura kwa elfu 80 kisha baadae mnananua kwetu kwa elf 8? hiyo ni sawa kweli?

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
November 6, 2020 at 10:26 AM delete

Suali la Kwanza .
Hivyo vifaav kujengea hilo Banda NI juu yenu au mfugaji.?

Suali la pili.
SUNGURA ananyonyesha kwa muda gani watoto wake ?

Suali la tatu.
Kwa Nini SUNGURA anawivu sana?

Suali la nne.
Kwa Nini SUNGURA anafukia vitoto vyake baada kuzaa? Pia NI muda gani vitoto vinaanza kunyonya na muda gani vinakula majani baada kuzaliwa?
Suali la tano.
Kwanini mnawanyonya wakulima kwa kuwauzia SUNGURA Bei ya juu sana huku nyinyi mkinunua kutoka kwao Bei ndogo kabisa kutoka 80,000 _8,000?

Reply
avatar