Featured

JINSI YA KUZALISHA AZOLLA KWA CHAKULA CHA KUKU

Habari Ndugu Mfugaji popote pale ulipo, jifunze jinsi ya kuzalisha azolla kwa chakula cha kuku na Mkulimastar.
.
Kwa maeneo mengi sana hapa nchini imekuwa changamoto hupatikanaji pamoja na bei za vyakula vya kuku, na watu wengi wamekuwa wakipata wakati mgumu na kufanya ufugaji kuwa na changamoto nyingi na hata kuhahirisha kufanya ufugaji.
Bali sasa vitambue vyakula ambavyo mfugaji unaweza zalisha katika mazingira yake kwa lengo la kulisha kuku wake.
Vifuatavyo ni vyanzo vya chakula ambavyo vyaweza tumika kulisha kuku.
- MMEA WA AZOLA.
Huu ni mmea ambao hukua ndani ya muda mfupi na uweza lisha mfugo wako wa kuku na kuwapatia chanzo kizuri cha protini pamoja na viini lishe vinginevyo.
MAZINGIRA YA UZALISHAJI
- Eneo ambalo litatumika hakikisha lina funikwa vyema kuweza zuia upotevu mkubwa wa maji, na kuchanganyana na uchafu wa ain ayeyote.
- Eneo lisiwe na shughuli nyingine kuepuka kuchanganyikana na uchafu mwingine pamoja na sumu zingine.
Jinsi ya kuotesha.
1. Andaa bwawa square mita 18 kina futi 1.5   au chombo chochote chenye ukubwa wowote unao endana na ukubwa wa eneo ulilo nalo.
2. Kisha weka nailoni ngumu au turubahi ambalo lituzuia kupotea kwa maji Kunywea chinina  Baada ya hapo weka samadi udongo kilo 27-30  mbichi ya ng`ombe ambayo itachukua eneo la inchi 10, ondoa uchafu wote hutakao jitokeza baada ya kuweka samadi juu ya maji hayo.
3. kisha weka mbegu kiasi cha kilo tatu (3), katika bwawa hilo maalumu.
4. Baada ya azola kuota Subiri kuvuna baada ya siku 15 kwa Mara ya kwanza baada ya hapo utakuwa ukivuna kila baada ya siku 2-3 kwa zaidi ya mwaka anza kuvuna na kuwapatia kuku wako, baada ya hapo anza kulisha kulingana na wingi wa mifugo ulio nao.

NAMNA YA KUWALISHA.
Kuna namna mbili kuu za kuwalisha kuku,
1. Namna  ya kwanza kwa kuwapatia  kwa kuchanganya na vyakula vingine kwa kuweka azolla kilo 50, pumba kilo 25, na kilo 25 za chakula cha madukani/ ulichochanganya mwenyewe ili kupata kilo 100
2. Namna ya pili kwa kuwapatia Chakula cha Azolla tu bila chakula kingine.

Subscribe to this Blog via Email :

8 comments

Write comments
Pita
AUTHOR
April 13, 2019 at 8:53 AM delete

Mbegu kwa hapa Mwanza zinapatikana wapi?

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
February 14, 2020 at 7:38 AM delete

Kwa mahitaji ya mbegu ya azolla nitafute kwa no 0623063061

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
March 25, 2020 at 12:10 PM delete

Asante kwa elimu makini. Je mbegu za Azolla hupatikana wapi Arusha

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
September 14, 2020 at 7:36 PM delete

Habari, nahitaji mbegu ya azolla dar nitaipata wapi??

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
January 2, 2021 at 7:52 AM delete

Asante. Naishi kongo, mbegu ya azola inaweza kusafirishwa je hadi kongo ?

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
January 12, 2021 at 3:22 PM delete

Vp kwa Tabora mbegu znapatikana wap??

Reply
avatar