Featured

BATA MAJI NA FAIDA ZAKE KATIKA UFUGAJI


Habari Mfugaji unayesoma makala zetu za UFUGAJIMAKINI.. Leo tumekuja na makala hii inayoeleza machache kuhusu ufugaji wa Bata maji au Bata wachafu kama wanavyoitwa na wengi


Bata Hawa wanaitwa Bata maji kutokana na tabia yao ya kucheza na maji kwa muda mwingi. Pia Bata Hawa hawawezi Kula bila kuwa na maji pembeni.


FAIDA ZA UFUGAJI WA BATA MANI (URAHISI WAKE)
  1. Wanakua kwa haraka tofaut na kuku
  2. Utotoaji wake ni mzuri tofauti na kuku kwani mayai ya bata yana uwezo wa kutunza joto kwa muda mrefu
  3. Vifaranga wa Bata hawahitaji joto wakat wa ukuaji wao kwa sababu ya ngozi yao kuwa na manyoya mengi.
  4. Sio wepesi kushambuliwa na magonjwa kama kuku
  5. Hawahitaji uangalizi wa karibu kama kuku
  6. Wanataga mayai makubwa na yenye virutubisho asili( kiini cha njano)
  7. Wana kitoweo(nyama tamu)
  8. Wanafikia uzito mkubwa hadi kilo sita(6) kwa Bata dume
  9. Wanahimili mazingira yote ya joto na baridi.
  10. Soko lake ni la uhakika hasa kwa jamii zinazopenda nyama ya Bata kama vile Upareni
Ufugajimakini tupo kwajili ya kuhakikisha Mfugaji wa Bata anapata soko la uhakika na Yule anayehitaji Bata wa kufuga anapata ili kutimiza malengo ya kila mmoja
KARIBU UFUGAJIMAKINI TUKUHUDUMIE


Subscribe to this Blog via Email :

4 comments

Write comments
Lucas
AUTHOR
February 20, 2021 at 2:46 PM delete

Wekeni link ya group la whatsap kwa wafugaji bata

Reply
avatar
Lucas
AUTHOR
February 20, 2021 at 2:46 PM delete

Wekeni link ya group la whatsap kwa wafugaji bata

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
July 20, 2021 at 8:47 PM delete

Hata Mimi natamani kufuga mbata

Reply
avatar
October 5, 2021 at 2:40 PM delete

Mimi nina aina tofauti za bata ufugaji wa bata ni rahic zaidi kuliko ufugaji wa kuku changamoto yao ni wanakula kupita maelezo 😅

Reply
avatar