Chanjo mbalimbali za kukinga magonjwa zina utaratibu wake kitaalamu, kama namna ya utunzaji na
namna kuwapa kuku. Zifuatazo ni dondoo muhimu za kufahamu ili chanjo yako ifanikiwe;
1. Ukihifadhi chanjo yako hovyo hovyo bila kufwata maelekezo ya kitaalamu, chanjo hiyo inakua Sumu
badala ya kuwa kinga na tiba. Chanjo iliyohifadhiwa vibaya haiwezi kufanikisha matibabu. Chupa za chanjo
huwa zinakuwa na lebo au karatasi yenye maelekezo ya jinsi ya kutumia pamoja na tarehe ya mwisho ya
matumizi (Expire date). Usipochanja kuku wako vizuri, ugonjwa unaweza kuenea zaidi.
2. Vifaranga vilivyoanguliwa huweza kuwa na magonjwa mbalimbali yaliyotoka kwa Mama kuku, kupitia
yai. Kwa hiyo kuwachanja kuku walio na umri chini ya siku kumi (10) ni muhimu sana, kwa sababu itazuia
magonjwa ambukizi kwa vifaranga kadri wanavyokua.
3. Kila chanjo imetengenezwa kwa kuwekwa mahali sahihi kwenye mwili wa kuku, kuna baadhi huwekwa
kwenye macho, baadhi kwenye maji na baadhi huchomwa kwa sindano kwenye mabawa. Kwa hiyo
usibadilishe matumizi ya chanjo.
4. Usiwape chanjo kuku Waliokwisha kuugua [Isipokua kama kuna mlipuko wa ugonjwa wa
Laryngotracheitis au Fowl pox]
5. Hifadhi chanjo mahali salama pasipokua na joto & mwanga wa jua wa moja kwa moja.
6. Chanjo zilizo nyingi ni viumbe hai visivyoonekana kwa macho (Living micro-organisms) au chembe
chembe zinazotengeneza magonjwa (disease-producing agents), Kwa hiyo hifadhi chanjo zako kwa
Uangalifu.
7. Kama unatumia maji ya kunywa kuku kama njia ya kuwapa chanjo, hakikisha Unatumia maji yasiyokua
na chumvi na Chlorine, kwa sababu chembechembe au viumbe waliopo kwenye chanjo huharibiwa na hizo
kemikali.
8. Baada ya kutoa chanjo hakikisha unachoma au unavitibu (Kuosha na Kemikali inayoua vimelea vya
magonjwa, Disinfect) vifaa vyote ulivyotumia wakati wa kutoa chanjo. Ukifanya hivi utazuia kueneza
magonjwa kwa kuku wazima wasiokua magonjwa.