KUCHAGUA MAYAI KWA AJILI YA KUATAMIA
👍Tumia mayai yaliyotagwa si zaidi ya wiki mbili zilizopita.
👍Angua vifaranga kwa kutumia mama kuku, au kuku wengine wanaoatamia, au bata au mashine ya
kutotoreshea (incubator).
👍 Kwa kuku na bata hakikisha unawapa idadi ya mayai kulingana na ukubwa wa maumbile yao, yaani
lazima mayai yatoshe chini ya matumbo yao wakati wa kuatamia.
👍Baada ya kuangua mayai safisha maeneo ya kutagia pamoja na kutupa maganda ya mayai
yaliyoanguliwa.
👍Kama unatumia mashine ya kuangulia mayai, hakikisha unageuza mayai angalau kwa siku mara 3,
isipokua siku tatu za mwisho kuelekea kuangua vifaranga (Siku ya 1 hadi 18: Geuza mayai, Siku ya 19
hadi 21: Usigeuze mayai)