✍🏾KULEA VIFARANGA, KUTUNZA KUMBUKUMBU NA KUDHIBITI MAGONJWA
👍Wapatie maji safi na salama wakati wote.
👍Wapatie vyakula laini kama unga wa nafaka au mazao ya mizizi.
👍Waruhusu vifaranga watembee kwa uhuru, wakifikia wiki 3 au 4.
👍Wapatie vifaranga wako chanjo ya KIDELI wakiwa na umri wa siku 4 tangu kuzaliwa.
✍🏾 KUWEKA KUMBUKUMBU
Mfugaji anapaswa aweke kumbukumbu kimaandishi kwa kila anachokifanya kwenye mradi wake,
hii itamsaidia kumpa dira mfugaji kama anafuga kwa hasara au kwa faida. Mfano wa kumbukumbu
anazoweza kuandaa ni pamoja na Gharama za kuanzisha mradi, gharama za kendeshea mradi kama
chakula na usafiri, idadi ya kuku jike, Majogoo, vifaranga, idadi ya mayai yanayokusanywa kwa siku au wiki
au mwezi, Idadi ya mayai yaliyoanguliwa na taarifa nyingine muhimu.
✍🏾KUDHIBITI MAGONJWA KWA VIFARANGA
Udhibiti wa magonjwa mbalimbali ya vifaranga ni muhimu sana kwa mfugaji, udhibiti huo ni pamoja na
Kukinga vifaranga wako dhidi ya magonjwa ambukizi kwa kuwapa Chanjo mbalimbali pamoja na kuzingatia
usafi wa banda na chakula. Pia udhibiti wa magonjwa ni pamoja na kuwatibu kuku mara wanapoumwa.
Asilimia kubwa magonjwa yanayoathiri vifaranga ni yale yanayodhibitiwa na Chanjo, Kwa hiyo ukizingatia
utoaji wa chanjo kwa vifaranga wako kama inavyofaa kitaalamu, utaweza kidhibiti vifo vya vifaranga kutokana na
magonjwa kwa asilimia kubwa.